Napiga hodi!
Waungwana hupiga hodi kwa kila mahali wanapoingia na kuwakuta wenyeji wamejaa teeele!
Nami nimefanya hivyo huku nikiwa na mategemeo makubwa ya kukaribishwa ama kupokelewa kwa mikono miwili na wenyeji wangu ambao si wengine bali ni wana blogu!
Kwa kipindi kirefu nimekuwa mshabiki wa kuperuzi katika blogu mbalimbali na kuona jinsi watu wanavyoweza kuwasiliana ama kufahamiana kupitia blogu, mwanzoni nilihisi ni kitu kinachoweza kunibana sana na kuutumia muda wangu mwingi katika blogu, nikajihisi kushindwa!
Mungu si Athumani, nikajikuta nashawishika kuanzisha ya kwangu ili wengine nao wapate fursa ya kuziona kazi zangu, jamani naomba mnipokee ndugu yenu!
Kwa kifupi mimi ni mwandishi wa habari na mpiga picha wa gazeti la Sani la Tanzania, ambalo hutoka mara mbili kwa wiki yaani Jumatano na Jumamosi, ni hayo tu!

2 Comments:
mzawa!
karibu katika ulimwengu huu wa blog. ila kama nilivyokushauri, weka picha. mtembelee mwenzio maggid mjengwa uone mafanikio yake katika mjengwa.blogspot.com kisha nistue
karibu mzawa katika ulimwenhu huu wa blogu.Usikose kutupa vile vituko vya "Sokomoko"
Post a Comment
<< Home