Wednesday, December 20, 2006

Mawaziri Lowassa na Sumari!


Waziri Mkuu Lowassa na Naibu Waziri wa Kazi Jeremia Sumari wakiwa na wake zao wakisubiri kumpokea Rais Kikwete katika ukumbi wa Ubungo Plaza kulikofanyika sherehe ya harusi ya watoto zao, Pamela na Sioi!

Rais Kikwete Harusini!


Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika ukumbi wa Ubungo Plaza katika sherehe ya harusi ya watoto wa Mawaziri katika serikali yake yake.
Watoto hao wa Waziri Mkuu Edward Lowassa (Pamela)na Naibu Waziri wa Kazi Jeremia Sumari (Sioi)walifunga ndoa Jumamosi iliyopita Desemba 16, 2006! Mungu aijaalie ndoa yao idumu milele!

Tuesday, December 12, 2006

Siri ya umri wa Beyonce yafichuka!


Ikiwa zimepita siku chache tangu kukumbwa na tuhuma za 'kumwagwa' na mpenzi wake Jay Z, hivi karibuni mwanadada Beyonce Knowles ameibukiwa na tuhuma zingine za utata juu ya umri wake halisi.
Tuhuma hizo za aina yake zimedai kuwa, mwanamuziki huyo amedanganya mashabiki wake juu ya umri wake halisi, ambapo kwa kipindi kirefu amekuwa akijitambulisha kuwa na umri wa miaka 25 kutokana na kuzaliwa Setpemba 4 mwaka 1981, jambo linalodaiwa kuwa si kweli.
Ikadaiwa zaidi kuwa, umri halisi wa binti huyo ni miaka 32 kutokana na kile kilichodaiwa kwamba ni kuzaliwa mnamo mwaka 1974, huku tarehe na mwezi wa vikibaki kama alivyojitangaza.

Banza awajibika jukwaani!



Mwanamuziki Banza Stone akiwajibika jukwaani sambamba na mwanamuziki mwingine wa bendi ya African Stars au Twanga Chipolopolo, Angelo walipozindua albamu yao ya Hujafa Hujasifiwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumamosi Desemba 8, 2006

Banza Stone katika Uzinduzi!



Mwanamuziki nguli wa bendi ya African Stars Twanga Chipolopolo Ramadhani Masanja au Banza Stone akiingia ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee katika onesho la Uzinduzi wa albamu ya bendi hiyo inayokwenda kwa jina la Hujafa Hujasifiwa!

Monday, December 04, 2006

Haya kula Keki Amina!


Mheshimiwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Amina Chifupa Mpakanjia akilishwa keki na mumewe Mohamed Mpakanjia kwenye sherehe ya kumbukumbu ya miaka sita ya ndoa yao na miaka mitano ya mtoto wao Rahman Mpakanjia! Sherehe hiyo ilifanyika nyumbani kwao Sinza jijini Dar.